IQNA

Muqawama

Balozi wa Yemen Iran:  Yemen itaendelea kusaidia Wapalestina, Walebanon

17:53 - October 08, 2024
Habari ID: 3479560
IQNA - Balozi wa Yemen nchini Iran amesema taifa la Yemen litaendelea kuwa na msimamo thabiti katika kuunga mkono harakati za muqawama au mapambano ya Kiislamu huko Palestina na Lebanon.

"Ujumbe wetu kwa wapiganaji wa muqawama (nchini Palestina na Lebanon) ni kwamba hamko peke yenu na tutasimama upande wenu hadi ushindi wa mwisho," Ebrahim al-Dailami alisema katika hotuba yake kwa kongamano la 7 la kimataifa la mshikamano na watoto na vijana Wapalestina uliofanyika mjini Tehran siku ya Jumatatu.

"Njia ya mashahidi wa muqawama, juu ya Mashahidi wote Sayed Hassan Nasrallah na Ismail Haniyah, itaendelea hadi kukombolewa kwa al-Quds na sisi tunabaki bila kuyumba katika njia hii," alisema.

Ameongeza kuwa kuuawa shahidi wapiganaji kama Nasrallah hakutadhoofisha muundo wa harakati za upinzani.

Al-Dailami pia ameashiria shambulio la hivi karibuni la makombora la Iran dhidi ya utawala wa Israel na kusema operesheni hiyo iliyopewa jina la Ahadi ya Kweli II, ilifanywa ili kudhihirisha azma ya muqawama wa kukabiliana na utawala wa Kizayuni na kulipiza kisasi damu za mashahidi.

Aliendelea kusisitiza umuhimu wa kudumisha umoja kwenye njia ya upinzani.

Aliyehutubia pia kongamano hilo ni Ayatullah Mohammad Hassan Akhtari, Mkuu wa Kamati ya Kuunga mkono Mapinduzi ya Kiislamu ya Watu wa Palestina, yenye mfungamano na ofisi ya rais wa Iran.

Yemeni Envoy Vows Continued Support for Palestinian, Lebanese Resistance

Alitumai kuwa kongamano hilo litakuwa fursa ya kufikisha sauti ya watoto wanaodhulumiwa wa Palestina duniani na kuweka mikakati ya kuendeleza muqawama dhidi ya utawala unaoua watoto wa Israel.

 4241164

Habari zinazohusiana
Kishikizo: muqawama yemen gaza israel
captcha